Friday, 9 April 2010

WASHINDI WAFIKA NITASOMA LEO

Bw. Valentino J. Mhoja kutoka  Dar es salaam Institute of Technology   akipokea zawadi ya NITASOMA MOBILE 3 kutoka 4Layers (T) Ltd's  Levis Paul akikabidhi zawadi hio Kushoto ni Bi. Venancia Donald.


Bi.Venancia Donald akipokea zawadi ya NITASOMA  MOBILE 1 kwa niaba ya Witness Lucas wa Tumaini University Iringa. Akikabidhi zawadi hizo kulia ni Levis Paul Campaign & Marketing Manager  4layers (T) Ltd. Shughuli hio fupi ilifanyika leo  katika ofisi ya kampuni hio iliyoko Msasani Dar es salaam.


Akielezea zaidi Bwana Levis Paul alisema promosheni hio ya NITASOMA inakuja juu kwa kasi  ikiwa hii ni wiki ya tatu tangu kuanza rasmi 15.03.2010  ni matarajio yao kuchagua washindi watatu kwa vitabu vya sekondari, mwanafunzi mmoja simu ya mkononi na laptop katika wiki ya nne yaani  jumatatu ijayo.

Alitoa changamoto  kwa walengwa walio vyuoni na mashuleni  kushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi NITASOMA UNI,  au NITASOMA HIGH au NITASOMA SEC kwenda 15767 ili kushiriki katika promotion hii.
ELIMU KWANZA.

info.nitasoma.com
www.nitasoma.blogspot.comNo comments:

Post a Comment