Friday 26 March 2010

Hatimaye mhitumu kapata haki yake

Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi nchini imemtaka Ofisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bw. Juma Kaponda, kutoa mahudhurio ya kila siku ya mwanafunzi Israel Johnson yaliyokua yamezuiliwa.

Mkuu wa Chuo cha Ualimu wa Kilutheri mkoani Mbeya Bw. Andalalisye Mwaihabi, alizuia matokea ya mwanafunzi huyo kwa madai kuwa hakusoma miaka miwili chuoni hapo ngazi ya cheti jambo lilosababisha Katibu Mkuu kiongozi, Bw, Philimon Luhanjo kuingilia kati.

Katika barua yenye kumb. Na. TTDA.260/361/012/27 ya Machi 19 mwaka huu, Bw. Kaponda amefafanuliwa kwamba kutokana na vielelezo kukamilika bila kuwa na shaka lolote mwanafunzi huyo anastahili kupata matokeo yake nakuwa mhitimu kamili wa chuo hicho.

"Tatizo lake limedumu kwa muda wa miaka miwili, wizara imedurufu barua za tatizo hilo, muongoni mwa vielelezo ni mawasiliano ya mlalamikajina WIzara, TAMISEMI, NECTA, Katibu Kiongozi, Chuo, REO wa Mkoa wa Mbeya." ilieze sehemu ya barua hio iliyo sainiwa na Bi.Hellen Liwala kwa niaba ya bw.Luhanjo.

Katika taarifa hio Wizara ilimtaka bw. Kaponda kufaya mawasiliano na mkuu wa chuo hicho ili kumaliza utata uliokuwepo na hatimaye mhitimu huyo kupatiwa haki yake.

No comments:

Post a Comment