Friday 26 March 2010

WANAFUNZI WA IFM WAVAMIA BODI YA MIKOPO

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM jana walivamia ofisi za BOdi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) kwa lengo la kuishinikiza bodi hiyo kutoa mikopo inayoendana na ongezeko la Ada chuoni hapo.

Hatua hio imekuja baada ya uongozi wa chuo hicho kusisitiza kuwa gharama za ada ya masomo chuoni hapo haziwezi kupungua, kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Akitoa ufafanuzi kwa wanfunzi hao , Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Bodi hio Bw. Cosmas Mwaisobwa alisema bodi hiyo haiwezi kugharamia sehemu ya ada iliyoongezeka kwa kuwa ongezeko hilo halikuingizwa kwenye bajeti ya masomo mwaka 2009/2010


source: Majira Machi 26.2010

No comments:

Post a Comment